Mamlaka ya vitambulisho vya Mtanzania NIDA imesema
inakusudia kufungua Afisi za kudumu za usajili kila Wilaya za Unguja na Pemba.
Afisa Usajili
wa NIDA Zanzibar Said Kassim Mohd amesema vituo hivyo vitakuwa na jukumu la
waliokosa na walikuwa hawajfika umri baada ya kukamilika zoezi linaloendelea katika maeneo mbalimbali.
Akizungumzia kazi za uandikishaji wa vitambulisho hivyo katika Wilaya ya
Wete na Chake Chake Pemba amesema kazi hiyo inaendelea licha ya kuweko kwa
changamoto ndogo ndogo katika vituo vya uwandikishaji.
Akizungumza na
Wandishi wa Habari Said ameeleza kuwa baadhi ya wananchi wamekuwa wanakaidi
maelekezo yanayotolewa hali inayoleta ugumu katika kazi hiyo.
0 comments:
Post a Comment