April 23, 2014


 Jumla ya watu ishirini na nane wamefikisha mahakamani kwa kosa la kutumia madawa ya kulevya katika maeneo mbalimbali.

Kati wa watumiwa wamekutwa na nyongo za bangi 120 katika operesheni ya jeshi la polisi la mkoa wa Mjini magharibi ya kudhibiti vitendo vya uhalifu kupambana na vijana wanaouza madawa ya kulevya katika jamii.

Kamanda polisi wa mkoa huo Mkadam Khamis Mkadam amesema pia  maiti tatu zimeokotwa katika maeneo ya Bandari ya Malindi na katika kisiwa cha Chumbe.

 Amewataka wananchi kushirikiana na polisi kutoa matokeo ya uhalifu katika shehia ili kudhibiti vitendo hivyo visiweze kutokea katika jamii.

0 comments:

Post a Comment