Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ameiagiza Wizara ya Habari,
Utamaduni, Utalii na Michezo kuchukua hatua za dharura kukabiliana na
changamoto zinazolikabili Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC).
Amesema ni lazima kuwepo mipango
hio ili liweze kuendesha shughuli zake kwa mafanikio na kukabiliana ushindani
mkubwa wa kibiashara
Dkt Sheni Amesema serikali imeshatoa
fedha nyingi kwa Shirika hilo hivyo hakuna sababu ya kushindwa kujiendesha
kibiashara.
Amefahamisha kuwa serikali imewekeza
kwenye na matumizi ya teknologia ya kisasa ikiwemo mradi wa digital Network
hivyo hakuna sababu ya kusuasua mpango huo.
Ameziagiza taasisi za Serikali
kufanyakazi kwa uwazi katika kupanga na kugawana rasilimali fedha ili pia kufanikisha
utekelezaji wa malengo yaliyowekwa.
Amesema utaratibu huo ni njia pekee itakayosaidia kufikia malengo
yaliyopangwa na Wizara kwa ufanisi.
Rais wa Zanzibar ameyasema hayo alipokuwa
akizungumza na uongozi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo kwenye
kikao cha kutathmini utekelezaji wa mpango kazi na bajeti ya Wizara hiyo katika
kipindi cha miezi tisa kuanzia Julai 2013.
0 comments:
Post a Comment