April 23, 2014

Na Salum Vuai, MAELEZO
Mdhibiti magonjwa - Kitengo cha Chanjo Wizara ya Afya Bw. Abdulhamid Ame
 akitoa ufafanuzi kuhusu Chanjo wakati wa Mkuta na wandishi wa Habari.
WAKATI bara la Afrika linaanza wiki ya chanjo za kujikinga na maradhi kwa watoto kesho (April 24), Waziri wa Afya Mhe. Juma Duni Haji, anatarajiwa kuzindua wiki hiyo kwa upande wa Zanzibar.
Uzinduzi huo  unafanyika Tanzaia nzima na katika nchi zote za bara la Afrika, kwa Zanzibar umepangwa kufanyika kitaifa katika kituo cha afya Chumbuni Wilaya ya Mjini na shughuli kama hiyo itafanyika katika wilaya zote kumi Zanzibar kuanzia leo Aprili 24 hadi 30, mwaka huu.  
Akizungumza na waandishi wa habari  mjini Unguja, mratibu wa chanjo Zanzibar Yussuf Haji Makame, amesema  zoezi hilo linawalenga watoto wote walio chini ya miaka miwili ambao, ama hawakukamilisha chanjo au hawajapata kabisa katika awamu iliyopita.
Amefahamisha kuwa  huduma hizo zinatolewa kutokana na agizo la Shirika la Afya Ulimwenguni (W.H.O) iliyoagiza kutoewa chanjo hizo  wiki ya mwisho ya mwezi Aprili kila mwaka ikiwa na lengo la kuwakinga watoto na maradhi yanayoweza kuzuilika kwa chanjo ikiwemo polio, pepo punda surua na mengineyo. 
Afisa huyo amewataka wananchi  wenye watoto wa umri chini ya miaka mitano, kuwapeleka  vituoni na kuhakikisha wanapata chanjo hiyo na kumaliza dozi ili kuwakinga na maradhi hayo, na hivyo kuliwezesha taifa kuwa na kizazi chenye afya bora.
Akitoa takwimu za hali ya maradhi ya surua kwa mujibu wa utafiti wa W.H.O, Makame amesema mwaka 2011 vifo 158,000 vilivyosababishwa na ugonjwa wa surua viliripotiwa ambapo  vifo 430 vinalitokea kila siku sawa  na vifo 18 vinavyoripotiwa kwa  saa . 
Kwa upande wake, Afisa Mdhibiti Magonjwa katika kitengo cha chanjo Zanzibar Abdulhamid Ameir, amesema mpango huo wa chanjo barani Afrika ulioanza mwaka 2011 unatarajiwa kukamilika 2020 kwa mujibu wa malengo ya  W.H.O katika kumaliza  au kupunguza tatizo la maradhi ya watoto.

Baadhi ya wandishi wa Habari wakifuatilia kwa makini maelezo ya Mratibu wa Chanjo Zanzibar Bw. Yusuf Haji (hayupo pichani) kuhusu siku ya Chanjo Afrika katika ukumbi wa Mazsons Hotel Shangani Mjini Zanzibar.
Muandishi wa Habari wa Staa TV Abdallah Pandu akitaka ukiuliza swali kuhusu wiki ya Chanjo Afrika.(PICHA NA MAKAME MSHENGA WA MAELEZO ZANZIBAR)

0 comments:

Post a Comment