Mkurugenzi Mipango, Sera na Utafiti Wizara ya afya Zanzibar Abdullatif Haji. |
WIZARA
ya Afya Zanzibar, imesema itahakikisha hatua zilizofikiwa za kupunguza vifo vya
mama wajawazito na watoto wakato wa kujifungua zinakuwa endelevu ili kufikia
malengo ya millennia.
Mkurugenzi
Mipango, Sera na Utafiti katika wizara hiyo Abdullatif Haji, amesema katika
mkutano wa siku moja kufunga mradi wa miaka mitano uitwao MAISHA uliofanyika
katika hoteli ya Grand Palace Zanzibar, kuwa lazima juhudi za kuimarisha afya
ya mama na mtoto ziendelezwe.
Mkurugenzi
huyo amesema Zanzibar imepiga hatua imefanikiwa kupunguza vifo hivyo kutoka 377
mwaka 2012, hadi kufikia 221 kwa sasa.
Amesema
serikali itaendeleza mkakati huo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ukiwemo
mradi wa MAISHA uliosaidia kupunguza vifo hivyo kwa asilimia 50 katika visiwa
vya Unguja na Pemba.
“Lengo
letu ni kuhakikisha hakuna mzazi anayekufa wakati wa kujifungua wala kupoteza
kizazi chake,” amesisitiza.
Mkurugenzi
huyo amesema mradi huo unaosimamiwa na taasisi ya Jhpiego Zanzibar chini ya
ufadhili wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani USAID, umesaidia
kuwakomboa akinamama kwa kuwaelimisha juu ya umuhimu wa kujifungulia hospitali
pamoja na kuhudhuria kliniki katika kipindi chote cha ujauzito.
Amefahamisha
kuwa, vifo vya mama wajawazito na watoto vinaweza kupunguzwa na kumalizwa
kabisa, kama kutakuwa na mkakati madhubuti wa utoaji huduma endelevu na
uangalizi wa kutosha kabla na baada ya kujifungua.
Amesema
lengo la Wizara ya Afya, ni kuhakikisha vya mama wajawazito vinavyotokana na
uzazi pamoja na vya watoto wanaokufa wakati wa kuzaliwa, vinapngua hadi 150
ifikapo mwaka 2015.
Mapema,
Mkurugenzi Mkazi wa Jhipiego nchini Tanzania Maryjane Lacoster, ameeleza kuwa
mafaniko yaliyopatikana katika kuokoa maisha ya mama na watoto wakati wa
kuzaliwa, yametokana na msaada na ushirikiano wa Serikali katika mpango huo wa
miaka mitano, sambamba na ule wa taasisi nyengine nchini na zile za kimataifa.
Amesema
mafanikio hayo yameipa moyo Jhipiego kuendelea kufanya kazi kwa karibu zaidi na
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, sambamba na washirika wanaofadhili mpango
huo katika kuhakikisha Wazanzibari wanakuwa na afya bora.
Naye
Mwakilishi wa USAID nchini Tanzania Lisa Patel, ameishukuru Wizara ya Afya
Zanzibar, kwa kuupa ushirikiano mradi huo uliorahisisha wanawake kupata huduma
bora kutokana na vifaa vya kisasa wakati wa ujauzito, kabla na baada ya
kujifungua.
Kwa upande wake,
msimaizi mkuu wa mradi wa MAISHA Dk. Dunstan Bishanga, ameeleza kuwa, tangu
kuanzishwa mradi huo mwaka 2008, zaidi ya watoa huduma 250 Unguja na Pemba,
wamepatiwa mafunzo kuhusiana na jinsi ya kuwahudumia akina mama wajawazito na
watoto
0 comments:
Post a Comment