April 22, 2014


Mratibu wa Tamwa Zanzibar, Mzuri Issa
Vyama vya siasa nchini bado havijawapa kipaumbele cha kuwashirikisha wanawake katika kugombea nafasi za uongozi katika ngazi za maamuzi.

Mratibu wa Tamwa Zanzibar, Mzuri Issa, amesema mbali na kutolewa nafasi  za  viti maalum lakini uteuzi wa wanawake kugombea  haujatosheleza kufikia malengo ya usawa wa kijinsia katika kuleta maendeleo.

Ametolea mfano wa baraza la wawakilishi lenye jumla ya waumbe 86 na 26 tu wanawake na kati yao ni watatu tu ndio waliogombea majimboni.

Mratibu huyo amesema tatizo hilo limechangiwa hasa kutokana na kushindwa kuwekwa  misingi imara ya wanawake kuongoza kutoka ngazi za shina hadi taifa kupitia katika vyama vyao kama njia ya kuwajenga uwezo wa kugombea nafasi hizo.

Amefahamisha kuwa nchi kadhaa zimefanikiwa harakati hizo kutokana kuweka mikakati ya kuwaendeleza na kuwawezesha wanawake na wanaume bila ya upendeleo.

Alizitaja nchi hizo ni pamoja na Denmark, Sweeden kwa nchi za ulaya na Ghana, Msumbiji, Afrika ya kusini na Rwanda ambayo ushiriki wa wanawake katika bunge umefikia asilimia karibu 64.

0 comments:

Post a Comment