April 22, 2014





Magonjwa kisukari na shinikizo la damu  yanaongezeka Zanzibar kutokana na wananchi wengi kukosa  elimu ya kujikinga na kukabiliana na maradhi hayo.
Daktari Ntol Abraham Mulind kutoka hospitali ya muhimbili  amesema   tatizo hilo limekuwa ni moja ya chanzo cha  baadhi ya wagonjwa waliogundulika na maradhi hayo kuacha kula dawa au kufuata masharti wanayopatiwa na daktari.
Alikuwa akizungumza katika zoezi la kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya ugonjwa wa kisukari na shinikizo la damu katika jimbo la Kikwajuni  huko Kiswandui medical center Kisiwandui  zilizoandaliwa na Jumuiya ya Madaktari wanafunzi wa Tanzania TAMSA kwa kushirikiana na Wizara ya Afya Zanzibar.
Dkt Ntol ameelezea umuhimu wa viongozi na serikali kuaendeleza  siku za upimaji afya  ya jamii  ili kutoa tiba na elimu juu ya kujikinga na maradhi karibu zaidi na wananchi.
Takwimu za Wizara ya Afya Zanzibar zinaonyesha  asilimia 33% ya Wananchi wa  wanasumbuliwa na tatizo la shinikizo la Damu na asilimia 3.7Kampeni ya huduma za uchunguzi na matibabu kwa magonjwa wa kisukari na shinikizo la damu zimeendelea  kwa siku ya tatu katika maeneo mbali mbali  ya Zanzibar.
 Mbunge wa jimbo la Kikwajuni ambae ni balozi wa mradi huo Hamad Masoud Masauni amesema  utoaji wa huduma hizo amesema lengo kuu ni kusaidia wananchi kupata huduma muhimu za kiafya karibu yao.
Kampeni hiyo inaendeshwa katika mikoa yote ya Zanzibar imezinduliwa Jumamosi April 19, 2014 na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.









0 comments:

Post a Comment