Watu wawili wamefariki dunia kwa nyakati tofauti huko Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa huo Issa Juma Selman awataja watu hao ni mtoto wa miaka 10 Mcha Simai Shaame mkaazi wa Mgambo aliefariki baada ya kuingia kisimani na Issa Ali Haji mwenye umri wa miaka 57 mkaazi wa kinduni.
Amefahamisha kuwa marehemu Issa Ali Haji alikutwa amefariki katika msingi pembezoni mwa barabara ya kinduni na alikuwa anatafutwa na jamaa zake baada ya kutoweka nyumbani kwake tangu juzi.
Alfajiri ya jana April 20 Jeshi hilo pia liliokota mwili wa kijana mmoja mwenye umri wa miaka 25 anaeitwa Vuai Ali Vuai pembezoni mwa nyumba yao katika kijiji cha kitope wilaya ya kaskazini B akiwa ameshafariki.
0 comments:
Post a Comment