Serikali ya Zanzibar
imekisia kutumia shilingi bilioni 705.1 katika mwaka wa fedha wa mwaka 2014/2015.
Waziri wa Fedha Omar Yussuf Mzee amesema kipaumbele
zaidi mwaka huu kimewekwa
katika sekta afya, miundominu, maji na elimu ili
kupata maendeleo.
Alikuwa
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu muelekeo wa bajeti
ya mwaka wa fedha 2014/ 2015
itakayo wasilishwa katika kikao cha
bajeti ya Serikali ya Zanzibar kinachotarajiwa kuanza May 14 mwaka huu.
Waziri Mzee
amefahamisha kuwa serikali inatarajia kukusanya shilingi bilioni 399 kwa mapato
ya ndani na bilioni 305.3 kwa mapato ya nje ikiwemo misaada na mikopo.
Akizungumzia
kuhusu hali ya uchumi umekuwa kwa asilimia 7.4 mwaka
jana ikilinganishwa na asilimia 6.8 ya mwaka 2012.
Ameongeza kuwa pato la
mtu mmoja limeongezeka na kufikia
milioni 1 na elfu 77 kutoka milioni 1 na elfu 30 la mwaka 2012.
Waziri wa Mzee ameongeza pia mfumko wa bei
umepungua kutoka asilimia 9.4 kwa mwaka 2012 hadi asilimia 5 mwaka jana.
Amezitaja sababu zilizochangia kukuwa kwa
uchumi ni pamoja na huduma za hoteli na mikahawa na kilimo kwa zao la karafuu na mpunga.
Aidha amesem idadi ya watalii waliotembelea
Zanzibar kwa mwaka 2012 imefikia 169,
223 na kwa mwaka 2013 wametembelea 181, 301 sawa na asilimia 7.1.
0 comments:
Post a Comment