Omar Ali Shehe mwenyekiti wa PAC |
Kamati ya kudhibiti na kuchunguza hesabu za serikali ya baraza la wawakilishi imesema bado kuna matumizi ya mabaya ya fedha za umma katika baadhi ya taasisi za serikali.
Mwenyekiti wa kamati hiyo Omar Ali Shehe amesema ubadhirifu huo umeongezeka kutokana na serikali kushindwa kuchukuwa hatua licha ya kuweka udhibiti wa matumizi ya fedha zake.
Ameishauri kupunguzwa matumizi hayo yasiyo ya lazima ili fedha zitumike kwa mahitaji muhimu ya wananchi na kupunguza madeni yasiyokuwa ya lazima kwa baadhi ya taasisi za serekali.
Omar Ali Shehe alikuwa akizungumza wakati kamati hiyo kudhibiti na kuchunguza hesabu za serikali ilipotembelea kuangalia matumizi ya fedha katika taasisi za Wizara ya habari, utamaduni, utalii na michezo Zanzibar.
0 comments:
Post a Comment