Mamlaka ya maji Zanzibar ZAWA imetiliana saini na kampuni Don Consultant Limited ya dar –es –saalam mradi wa kuimarisha huduma ya maji na usafi wa mazingira katika wilaya ya mjini wenye thamani ya zaidi dola za Kimarekani milioni 2.
Mkurugenzi mkuu wa ZAWA Dk Mustafa Ali Garu amesema Mradi huo wa miaka minne utahusika katika ujenzi wa visima vya maji na ufukuaji wa mabomba ya zamani ya Mji mkongwe pamoja na ujenzi wa vyoo katika baadhi ya skuli zilizomo ndani ya mji huo.
Nae mshauri muelekezi wa kampuni ya Don laurent mzee sechuo ameahidi kutekeleza mradi huo kwa mujibu wa makubaliano kutokana na umuhimu wa mji huo katika kusaidia maendeleo ya Zanzibar.
0 comments:
Post a Comment