Makubaliano hayo yametiwa saini na Balozi maalum wa EU
nchini Tanzania Filiberto Ceriani
na na katibu mkuu Wizara ya Ardhi Maji
ujenzi na nishati Al halil Mirza kwa
upande wa serikali ya Zanzibar.
Akizungumza katika hafla hiyo mjini Zanzibar balozi Ceriani
amesema mradi huo wa miaka mitano utaiwezesha zanzibar kuwa na vyanzo mbadala
vya kuzalisha umeme utasaidia kupunguza umasikini na kuimarisha uchumi
wake.
Amesema EU imesaidia mradi huo ili kuisaidia Zanzibar kukabiliana na matatizo mbali mbali ya
ukosefu wa huduma hiyo na kupunguza shughuli zinazosababisha mabadiliko ya
tabia nchi hasa kwa wananchi wa vijijini.
Naye katibu mkuu Wizara ya ardhi maji ujenzi na
nishati Al halil Mirza amesema mbali na shughuli za utafiti huo umeanza ili
kujua umeme wa jua na upepo utakapotumika na inaweza kutumia umeme wa kibiashara.
0 comments:
Post a Comment