Mratibu wa Dawati la jinsia la wanawake na watoto makao makuu ya Polisi Maua Saleh Juma |
Vielelezo kadhaa vya ushahidi wa kesi za udhalilishaji vimetelekezwa
katika kituo cha Mkono kwa mkono kwa mkono (One Stop Center) kilichopo
Hospitali kuu ya Mnazimmoja.
Mwandishi wa habari hizi alishuhudia kuwepo kwa vidhibiti
hivyo vya watu kadhaa vya waliofanyiwa udhalilishaji ikiwemo ubakaji katika
maeneo tofauti ya visiwa hivi.
Vidhibiti hivyo ni pamoja na nguo za ndani za waliofanyiwa vitendo
hivyo vinavyotakiwa kuchukuliwa na polisi kwa ajili ya kuendeleza uchunguzi
wa kesi hizo.
“Vidhibiti hivi vimekaa kwa muda mrefu hapa bila ya kupelekwa
kufanyiwa uchunguzi wa kitaalamu wa vinasaba (DNA) kukamilisha ushahidi” amesema
Marijan Msafiri ambae ni Daktari dhamana wa kituo hicho cha Mnazimmoja.
Amefahamisha tabia hii inasababisha kesi za udhalilishaji
ikiwemo ubakaji kuchelewa au kukwama kwa vielelezo jambo linalorejesha nyuma watendaji
wa taasisi nyengine za kupambana na vitendo vya udhalilishaji Zanzibar.
Akitoa maelezo Mratibu wa Dawati la jinsia la wanawake na
watoto makao makuu ya Polisi Maua Saleh Juma amekiri kuchelewa kuvichukuwa vidhiviti
hivyo katika kituo hicho cha mkono kwa mkono na wao wanawajibu kuvichukua
vielelezo hivyo ili kuvifanyia kazi na haki ya kisheria kufuata mkondo wake.
“ mimi niliwahi kushuhudia vielelezo hivyo lakini nikiri kuwa
ni udhaifu wa kiutendaji kwa jeshi letu ”, amesema Maua.
Ameongeza kuwa jeshi la polisi ndilo lenye jukumu la
kuvichukua vidhibiti hivyo ili kufanyiwa
uchunguzi na kumtia hatiani watuhumiwa wa matendo hayo.
Hata hivyo amekiri kuwepo changamoto kubwa katika jeshi la
polisi ikiwemo usafiri wa na fedha kwa
ajili ya kupeleka vielelezo hivyo kwa uchunguzi wa vinasaba (DNA) Dar-es-Salaam
na kuendeleza kesi hizo.
Mratibu Maua akizungumzia kuhusu madai ya baadhi ya polisi kusaidia
usuluhishi wa makosa ya udhalilishaji ikiwemo ubakaji ameeleza kuwa ni kosa Kuhusiana
na madai ya baadhi ya polisi kufanya suluhisho, kwa makosa ya udhalilishaji
ikiwemo ubakaji
“Kitendo cha polisi ni kosa la kisheria na kumtaka Mtu yoyote
aliekuwa hajatendewa haki na polisi amehusika kwa njia moja au nyengine kuwasilisha
malalamiko yake ngazi za juu ya polisi kwa ajili ya kuchukuliwa hatua.” amesema
Mratibu wa dawati la jinsia Makao makuu ya polisi Zanzibar.
baadhi ya waandishi wakibadilishana mawazo na Mratibu wa Dawati la jinsia la wanawake na watoto Maua Saleh Juma |
0 comments:
Post a Comment