Rais wa Zanzibar
na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, amekutana na
kufanya mazungumzo na uongozi wa kampuni ya ZANTEL
ukiongozwa na Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Millicom Group, Mauricio Ramos, ikulu
mjini Zanzibar
Katika
mazungumzo hayo rais Shein ameeleza haja kwa kampuni ya ZANTEL kupitia kuimarisha utoaji huduma zake ili kupata
mafanikio zaidi katika ushindani wa kibiashara.
Amesema iwapo kampuni hiyo itafanikiwa katika
utoaji huduma zake ndani na nje ya nchi kutasaidia kuitangaza Zanzibar kimawasiliano
na kuinua uchumi wa Taifa
Dr. Shein amesema serikali ya Zanzibar itaendeleza
ushirikiano wake na kampuni hiyo ambyo serikali ina hisa zake.
Nae Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Millicom Group, Mauricio Ramos, amesema kampuni hiyo
itahakikisha ZANTEL inapata mafanikio zaidi kutokana na mikakati madhubuti
iliyowekwa hasa katika kuimarisha miundombinu yake ili kutoa huduma za uhakika.
 |
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein (kulia) akisalimiana na Bw,Mauricio Ramos,Mtendaji Mkuu wa kampuni ya
"Millicom Group"akiwa na ujumbe wake walipofika Ikulu Mjini Unguja
kwa mazungumzo leo (kushoto) Nd,Benoit Janin Mtendaji Mkuu wa Zanztel
23/08/2016.
|
 |
Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia)
akisalimiana na
Bibi Rachel Samren Naibu Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Millicom Group
pia
Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Zanztel (katikati) Bw,Mauricio Ramos,Mtendaji Mkuu wa
kampuni
ya "Millicom Group"(wa pili kulia) na (kushoto) Nd,Benoit
Janin Mtendaji Mkuu wa Zanztel ujumbe huo ulifika Ikulu Mjini Unguja leo
kwa mazungumzo na Rais leo 23/08/2016
|
 |
Mkurungenzi Mtendaji wa Millicom
Group Mauricio Ramos akifurahia zawadi aliyokabidhiwa na wanafanya kazi wa
kampuni ya simu za mkononi ya Zantel Zanzibar baada ya kufanya ziara ya
kutembelea ofisi za kampuni hiyo Zanzibar.
|
 |
Mkurungenzi Mtendaji wa Millicom
Group Mauricio Ramos akiwa kwenye ya pamoja na wanafanya kazi wa kampuni ya
simu za mkononi ya Zantel Zanzibar baada ya kufanya ziara ya kutembelea ofisi
za kampuni hiyo Zanzibar.
|
0 comments:
Post a Comment