Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande
Othuman ametoa siku saba kwa mahakimu 508 watoe maelezo ni kwanini
wasifunguliwe mashtaka ya nidhamu na kuwajibishwa, baada ya kufanya kazi chini
ya kiwango.
Jaji Mkuu Chande ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari
katika Viwanja vya Mnanzi Mmoja jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya
kuadhimisha Wiki ya Sheria.
Amesema kiwango cha kesi kwa kila Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi na Mahakama ya Wilaya ni 250, ambapo Mahakimu Wakazi 121 kwenye mahakama hizo wameamua kesi chini ya 100 mwaka jana.
Amebainisha kuwa kiwango cha kwa kila Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo ni 260, ambapo mahakimu Wakazi na Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo 387 wameamua kesi chini ya 100 mwaka jana.
"Ukiondoa wale ambao wameajiriwa karibuni, wanaofanya kazi kwenye mahakama za mwanzo zisizokua na mashauri mengi au waliyokwenda masomoni kati kati ya mwaka au likizo za ujauzito hawatahusika katika sakata la kujieleza.

"Majaji Wafawidhi nimewaagiza
wachambue na kuanisha mahakimu wote walioshindwa kufikia kiwango cha kesi
walizopaswa kuamua kesi 250 na kesi 260 kwa mwaka jana na kuwataka watoe
maelezo ndani ya siku saba kwa nini wasichukuliwe hatua," amesema Jaji
Chande
Jaji Chande alitoa muda wa
kukamilika kwa mchakato huo, ambapo walizitaka idara husika ndani ya siku 21
kila kitu kiwe kimekamilika ili ijulikane ni hatua gani wanachukuliwe.
"Mahakama haikubali hakimu
ambaye anabembeleza kesi. Hakimu hatakiwi kufanya hivyo anatakiwa asikilize
kesi hizo naazimalize. Haiwezekani katika mahakama moja hakimu mmoja anamaliza
kesi 800 mwingine anamalizia chini ya 100 hilo halitakubalika kutokana na kasi
ambayo tunayo," amesema
Jaji Mkuu Chande ameema mahakimu hao
watapelekwa katika kamati zao kwa hatua ya kujieleza. Kazi kuu ya kamati hizo
ni kupeleleza, kuchunguza na kushughulikia mashtaka yote ya nidhamu ya
mahakimu.
"Mahakimu wote walioshindwa kufikia malengo ya mwaka la kesi na kushindwa kutoan sababu za kuridhisha kwa nini wameamua idadi ndogo ya kesi kuliko walivyopaswa, ambapo itashughulikiwa haraka na Kamati za Maadili za Mahyakimu kwa mujibu wa sheria na taratibu za haki," amesema

Hata hivyo, Jaji Mkuu Chande amewapongeza
mahakimu waliovuka kiwango, ambapo mahakimu 14 wameamua zaidi ya kesi 700 kwa
mwaka jana na mahakimu wengine wamesikiliza kesi 915,789 na 778.
Amesema mkakati wao ni kuanza kesi sifuri mwaka unapoanza, kwa sababu kuna baadhi ya mahakama za mwanzo zimekuwa zikimaliza kesi na kuanza mwaka upya.
Amesema mkakati wao ni kuanza kesi sifuri mwaka unapoanza, kwa sababu kuna baadhi ya mahakama za mwanzo zimekuwa zikimaliza kesi na kuanza mwaka upya.
Jaji Mkuu Chande alisema Januari 1,
2015 mahakama za mwanzo zilianza na kesi 34,126 na mwaka huu Januari 1 zilianza
na kesi 20,431. Kiwango cha kumaliza kesi ukilinganisha na idadi ya kesi
zilizosajiliwa 2015 nni zaidi ya asilimia 100. Mahakama ya Mkuranga asilimia
141, Rufiji asilimia 121 na Bukoba Mjini asilimia 224.
0 comments:
Post a Comment