March 09, 2016

Jumla ya wagonjwa 1974 wameambukizwa  maradhi ya kipindupindu na kati yao 22 wamefariki dunia tangu kuzuka kwa ugonjwa huo Zanzibar mwezi wa Septemba mwaka 2015 na 31 wanaendelea kupatiwa matibabu hadi sasa .
Daktari dhamana kanda ya Unguja Dkt. Fadhil Mohammed  Abdallah amesema bado ugonjwa huo ni tatizo na ameomba juhudi zaidi kuchukuliwa ili  wananchi wawe  na mwamko wa kuchukua tahadhari kuhusu kujikinga na maradhi hayo.
Akizungumza na waandishi wa habari katika semina ya waandishi wa habari juu ya kipindupindu mjini Zanzibar daktari mkuu kanda ya Unguja Dkt Fadhil Mohamed abdalla mwamko huo utaifanya zanzibar kuwa salama.
Dkt. Fadhil Amesema kipindupindu huambukizwa na maji yaliyochanganyika na kinyesi cha binadamu ambapo kwa mujibu wa utafiti uliofanywa unainesha asilimia kubwa ya maji yanayotumika Zanzibar yana vimelea vinavyosababisha maradhi hayo.
Amezitaja tahadhari  hizo ni pamoja na kuweka  mazingira  safi, kufuata  masharti ya afya,  kuchemsha maji ya kunywa  ama kutumia maji yaliyotiwa dawa ya kuulia bektiria wanaosababisha maradhi hayo.
Hivyo Dkt. Fadhil amewasisitiza wananchi kuacha tabia ya kula ovyo njiani, kukosha matunda na mboga mboga kabla ya kula na kuchukua tahadhari kubwa wakati wa kumshughulikia maiti ya maradhi ya kipindu pindu kwani  ni miongoni mwa njia za maambukizi ya maradhi hayo.
Aidha amewataka waandishi wa habari kutekeleza majuku yao katika kutoa elimu kwa wananchi ili  wafahamu zaidi dhidi ya kukabiliana na maradhi hayo.
 “Waandishi wa habari  mnao mchango mkubwa wa kutoa elimu  kwa jamii  katika kukabiliana na maradhi ya kipindupindu  hivyo  tunategemea ushirikiano makubwa kutoka kwenu,” amesisitiza  Dkt. Fadhil
Akifungua mafunzo hayo Mkurugenzi  Mtendaji Kamisheni ya kukabiliana na Maafa Zanzibar Ali Juma  Hamad amesema juhudi za pamoja zinahitajika kwa  mtu na taasisi katika kukabiliana na kipindupindu kwani si jambo la kawaida kuwepo kwa muda mrefu.
Akiwasilisha mada ya majukumu ya vyombo vya Habari katika kudhibiti miripuko ya maradhi ya kuambukiza, Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo  Zanzibar Rafii Haji Makame  amesema vyombo hiyo vinajukumu la lazima katika kusaidia umma kudhibiti vifo na athari nyengine za kiuchumi na kijamii zinazosababishwa na miripuko ya maradhi .
Hivyo ametaka kuongezwa ushirikiano kati ya vyombo vya habari na sekta ya afya ili kupata taarifa sahihi kwa wakati katika kufikisha ujumbe kwa umma.
mapema mwakilishi wa shirika la Afya Dunuia (WHO) Andemichael Ghirmay amesema maradhi ya kipindupindu ni rahisi sana kukabiliana nayo kuliko maradhi mengine ya miripuko iwapo kutakuwa na mikakati ya pamoja kati ya taasisi mbali mbali zinazoshughulikia mazingira na usafi wa mji.
Wakati huo huo Katibu wa Jumuiya  ya maafisa wa afya Zanzibar Ahmed Suleiman Saidi amewashauri wananchi wa shehia ya Shaurimoyo kubadili tabia na kuweka mazingira wanayoishi katika hali ya  usafi ili kujikinga na kipindupindu.
Ametoa ushauri huo alipokuwa akizungumza na wananchi wa shehia hiyo walipowatembelea kutoa taaluma  juu ya maradhi hayo kutokana kuwa ni miongozi kati ya shehia zilizoathirika na kipindupindu.
Washiriki wa mafunzo hayo wakimsikiliza  kwa makini Daktari 
dhamana Kanda ya Unguja Dkt. Fadhili Mohamed alipokuwa 
akielezea njia za kukabiliana na kipindupindu.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Rafii Haji Mkame
akiwasilisha mada ya wajibu wa waandishi wa habari katika  kukabiliana na
maradhi ya miripuko Zanzibar

Katibu wa Jumuiya ya Maafisa wa Afya Zanzibar Ahmed Suleiman Said
 akitoa elimu ya kupambana na maradhi ya kipindupindu kwa wananchi wa shehia ya 
Shaurimoyo Mjini Zanzibar. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

0 comments:

Post a Comment