December 02, 2015


Meli mpya ya Serikali ya Zanzibar Mv  Mapinduzi II imewasili bandari ya Zanzibar.


Meli hiyo imetengenezwa Meli hiyo imetengenezwa Korea ya kusini kwa gharama ya dola za Kimarekeni milioni 30.6.

Mv Mapinduzi II ina uwezo wa kupakia abiria  wasiopunguwa 1,200 pamoja na tani  200 za mizigo itakuwa ikifanya safari zake Pemba pamoja na Dar es-Salam.
Kufika kwa meli hiyo kunaonekana kutapunguza tatizo la usafiri na inaelezewa kuwa itaanza kazi zake hivi karibuni mara tu baada ya kukamilika taratibu za uhakiki.
MV Mapinduzi II ilitarajiwa kuwasili Zanzibar  Julai 2015 ilikwama nchini Mauritus kufuatia kuwekewa kuzuizi na kampuni ya Leomthong  ya Thailand iliyokuwa inaidai Shirika la Biashara za Nje Zanzibar BIZANJE lililokuwa linaingiza vyakula na bidhaa mbalimbali katika miaka ya 80.


                  

0 comments:

Post a Comment