Jumla ya watu 82 wamegundulika kuambukizwa virusi vya Ukimwi kati ya watu
16,160 waliopima kwa hiari Pemba.
Takwimu hizo zimetolewa na Afisi ya programu ya kudhibiti Ukimwi Pemba ZACP
zinaonesha watu hao wamegundulika kuanzia Januari hadi Septemba 2015 baada ya
kupima katika shughuli mbalimbali za uhamasishaji juu ya Ukimwi.
Takwimu za jumla zinaonesha kuwa maambukizi ya ugonjwa huo Pemba imefikia asilima 3 lakini kwa kuangalia
makundi maalum inakisiwa kufikia zaidi ya asilimia 5.
Kundi la vijana ndio linaloonekana kuathirika zaidi na maambukizi mapya
kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo
vishawishi miongoni mwao na ngono zembe.
Suala la usiri pia limetajwa kuwa ni changamoto inayotatiza juhudi za
taasisi na jamii katika kutoa elimu kuhusu Ukiwmi kwa makundi mbalimbali
kisiwani humo.
Taarifa hii imetolewa na mratibu wa kitengo cha
mradi huo wa ZACP.
"zanzibar leo
0 comments:
Post a Comment