Umoja wa Vijana wa Chama
Cha Mapinduzi (UVCCM ) umesema ushindi alioupata mgombea wa CCM Rais Dk
Ali Mohamed Shein kwamba ni kielelezo cha kuimarika kwa msingi ya demokrasia
Zanzibar na kukubalika kwa mgombea huyo kwa wapiga kura na wananchi wa Zanzibar
.
Umesema ushindi huo sasa
umehitimisha mvutano na maneno yaliyokuwepo ambayo yalikuwa yakienezwa kwa
makusudi , kupotoshwa na baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani
visiwani humu.
Kaimu Katibu mkuu wa
UVCCM Shaka Hamdu Shaka ameeleza hayo Afisi kuu ya UVCCM Kikwajuni wakati
akizungumza na wandishi wa habari mara baada ya kumaliza kwa maandano makubwa
yaliyoandaliwa na UVCCM kusherehekea ushindi wa CCM uliotangazwa na
Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi Zanzibar Jecha Salim Jecha kulitangaza
jina la Dk shein mshindi wa uchaguzi huo.
Alisema
ushindi alioupata Dk shein kwa kupata jumla ya kura 299982sawa na
asilimia 91.4 kumeidhihirisha dunia jinsi ya kukubalika kwa kiongozi huyo
katika aina ya utawala na uongozi wake.
"Ameonyesha
umahiri, upeo na uwezo mkubwa katika kuongoza serikali ya umoja wa
kitaifa kwa miaka mitano iliopita; amekuwa mstahamilivu na nguzo muhimu ili
jamii isiendelee kugawanyika "alisema shaka
Kaimu Katibu
Mkuu alisema aina ya uongozi wa Rais Dk Shein ni wa kipekee na kwamba kama
angekuwa si mtawala mwenye maarifa mapana na uvumilivu wa kisiasa serikali hiyo
anaamini ingevunjika mapema.
Shaka alisema
serikai za mseto za Zimbabwe na Kenya ziliweza kuyumba na kwamba
hazikudumu kutokana na baadhi ya viongozi wake kukosa kuaminiana, kuvumiliana
na kustahamiiiana .
"Ushindi
huu ni pigo jipya kwa chama cha CUF ambacho kimesusia uchaguzi wa marudio bila
sababu za msingi, ushindi wa Dk shein naamini utaleta mageuzi makubwa ya
kiuchumi na kuishangaza dunia katika maendeleo ya demokrasia
"alisems Shaka
Aidha alisema
anatarajia serikali mpya ijayo haitakuwa na viongozi wababaishaji na badala
yake watateuliwa wazalendo, wachapa kazi na watu wenye uchungu wa kiyatetea Mapinduzi
bila kushiriki usaliti.
Hata hivyo
Shaka alisema anaamini kuwa chini ya uongozi wa kipindi cha pili cha utawala Dk
Shein na sera makini za ccm ,ataendelea kusimamia uadilifu serikalini,
kujenga umoja wa kitaifa nchini pamoja na kuwatumikia wananchi ipasavyo
na kudumisha huduma za jamii .
"UVCCM
tuna matumaini makubwa na na Dk shein katika awamu mpya ya ushindi wake;
ataunda baraza la mawaziri makini, na hatutosita kumpongeza kila atakapofanya
vizuri pia hatutakaa kimya pale tutakapoona mambo hayaendi ipasavyo
"alisema .
Shaka
anewahimiza vijana mahali popote walipo kumuunga mkono Dk shein na kuisaidia
serikali yake ili iweze kupiga hatua za kimaendeleo na kwamba hatawaangusha
katika uongozi wake.
"Tunahitaji
kutoka mahali tulipo na kufika tunakotarajia, tungependa kuona uwajibikaji
mpya,utendaji wenye kubeba dhamira na utekelezaji wa malengo na sera hivyo ni
wazi kuwa wapatikane watu wenye uwezo na upeo ya kukwamua nchi mahali
ilipo sasa"
0 comments:
Post a Comment