RAIS wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein leo amemuapisha
Bwana Said Hassan Said, kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na
Mwenyeikiti wa Baraza la Mapinduzi alimteua Bwana Said Hassan jana kushika
wadhifa huo kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu cha 55 (1) cha Katiba
ya Zanzibar ya mwaka 1984.
Hafla ya kumuapisha
Mwanasheria Mkuu huyo ilifanyika Ikulu Mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na
viongozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Miongoni mwao ni Jaji
Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu, Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa
Baraza la Mapinduzi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe.
Abdalla Mwinyi Khamis.
Wengine ni Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali, Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Mahmoud Mussa Wadi, Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar Khatib Abrahman Khatib, Washauri wa Rais wa wengine wa Serikali.

0 comments:
Post a Comment