Mradi wa PartoMa unaoshirikisha Chuo Kikuu cha
Copenhagen nchini Denmark na Hospitali Kuu ya Mnazimmoja wenye
lengo la kuongeza ufanisi na kuwajengea uwezo wafanyakazi wa wodi
za wazazi katika hospitali ya Mnazimmoja umeanza kuleta mafanikio
makubwa.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na mradi wa PartoMa kwa
kushirikiana na Taasisi isiyo ya kiserikali Kanga Martenity Trust (KMT) iliyopo
Hospitali ya Mnazimmoja umeonyesha vifo vinavyotokana na uzazi
na vifo vya watoto wanaozaliwa vimepungua tokea kuanza kwa mradi huo
mwaka mmoja uliopita.
Akiwasilisha utafiti uliofanywa na mradi wa PartoMa
ambao uliwashirikisha madaktari, wakunga na wasaidizi wakunga katika wodi za
wazazi, Dkt. Anna Maaloe amesema bado ni mapema kuthibitisha kuwa mafanikio
hayo yanatokana moja kwa moja na kuwepo mradi huo lakini ufanisi na
utaalamu wa wafanyakazi kwenye wodi za wazazi Hospitali ya
Mnazimmoja umeongezeka.
Amesema Hospitali za rufaa, kama ya Mnazimmoja zinawajibu
mkubwa wa kuwa na mafunzo ya mara kwa mara kwa wafanyakazi waliopo na
wanaotegemewa siku za mbele na kuweka miongozo bora ili kuokoa maisha ya mzazi
na mtoto pamoja na wagonjwa wa kawaida.
“Kwa kuliona hilo mradi wa PartoMa umekuwa ukiandaa mafunzo
ya kuwajengea uwezo madaktari na watendaji wa wodi za wazazi
Hospitali Mnazimmoja siku moja kwa miezi mitatu baada
ya saa za kazi na kuweka miongozo ambapo wafanyakazi wengi
wamekuwa wakishiriki,” aliongeza Dkt. Anna.
Katika utafiti huo Dkt. Anna amesema imebainika
kuwa wafanyakazi wengi wa Hospitali ya Mnazimmoja wamehamasika kuongeza
elimu na ufanisi na hiyo inasaidia katika kuokoa maisha ya wananchi.
Hata hivyo amesema bado kunachangamoto katika kutoa huduma
bora zaidi katika Hospitali ya Mnazimmoja ikiwemo uhaba wa wafanyakazi
katika wodi za wazazi ukilinganisha na ongezeko kubwa la wazazi
wanaotumia Hospitali hiyo.
Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika Hoteli ya Tembo
Forodhani, Mwenyekiti wa KMT Dkt. Mohammed Hafidh amesema utafiti huo ambao ni
wa kwanza kufanywa na kuwashirikisha watafiti wa wazalendo Hospitali ya
Mnazimmoja utasaidia kuwa na taarifa sahihi na za uhakika kwa maendeleo ya
Hospitali hiyo.
Amesema lengo la utafiti huo ni kuwasaidia mama wajawazito
kujifungua salama na kwa heshma na kuzuia vifo vya mama na mtoto ambavyo
vinaweza kuzuilika.
Nae Dkt. Naufal Kassim amekiri kuwepo mtafartoMa na
ameshauri madaktari kujipanga kufanya tafiti zaidi za afya na kuyatumia
matokeo ya tafiti zilizopo kwa ukamilifu.
Katika hafla hiyo Dkt. Ali Salum kwa niaba ya
Mkurugenzi wa Hospitali Kuu ya Mnazimmoja aliwakabidhi vyeti madaktari,
wakunga na wasaidizi wakunga walioshiriki mafunzo ya kuwajngea
uwezo baada ya saa za kazi bila malipo katika hospitali hiyo.
Mtafiti kutoka Mradi wa PartoMa Dkt. Anna Maaloe akiwasilisha utafiti wake
juu ya huduma za wodi za wazazi za Hospitali kuu ya Mnazimmoja.
|
0 comments:
Post a Comment