March 13, 2016

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)  Kimemteuwa  Dkt  Vicent Machinji kuwa Katibu Mkuu mpya wa Chadema hicho.
Katika Kikao hicho cha Baraza Kuu, Freeman Mbowe alitangaza jina la Dk. Machinji na kuungwa mkono na wajumbe wa baraza hilo, hivyo anajaza nafasi iliyoachwa na Dk. Willibrod Slaa, aliyejienguwa ukatibu mkuu wa chama hicho.
Nafasi ya Katibu wa Chadema ilikuwa wazi tangu Dk. Slaa alipoondoka Chadema muda mfupi baada ya chama hicho kumpitisha Edward Lowassa aliyetokea CCM kuwa mgombea urais wa chama hicho na kuungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

0 comments:

Post a Comment