March 12, 2016

Watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo wamechoma moto nyumba saba pamoja na kituo cha Afya cha kiuyu Minungwini katika Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Matukio hayo yametokea majira ya saa nane usiku yamehusisha nyumba mbili katika shehia ya Kangagani, nyumba mbili micheweni na moja katika kijiji cha Gando.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskaziuni Pemba Hassan Nassir Ali amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa nyumba hizo zimechomwa moto kwa kutumia mafuta ya taa.
Ameongeza kuwa hakuna mtu aliejeruhiwa katika matukio hayo na jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi kuwabaini waliofanya tukio hilo ili kuwafikisha ktika vyombo vya sheria..
Amewataka wananchi kuendelea kuwa watulivu huku jeshi la Polisi likiimarisha ulinzi.
Mmoja wa wananchi walichomewa nyumba yao  Hadia Faki Ali wa kijiji cha Kangagani amesema yeye na watoto wake saba walikuwa wamelala na wameshtushwa baada kuongezeka joto kali ndani ya nyumba yao walipotoka nje  walibaini kuwa nyumba yao inaungua.
Hata anashkuru kwa kuwa wote walitoka salama hakuna aloungua ingawaje vitu vyao vyote vimeteketea kwa moto huo.
Wakati huo huo kufuati kujitokeza kwa matukio hayo Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mh, Omar Khamis Othman amepiga marufuku mikusanyiko ya vikundi katika maeneo mbali mbali kuanzia saa mbili za usiku.
Matukio ya uchomaji wa moto nyumba za wananchi na maskanii za vyama vya siasa yamekuwa yakishamiri hivi sasa kisiwani Pemba na sababu kubwa inadaiwa kuwa ni masula ya kisiasa.

0 comments:

Post a Comment