Makamu wa
pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif
Iddi amesema mwananchi
hasa vijana hawezi kuwa mzalendo kama hajajifunza historia ya taifa lake.
Amefahamisha kuwa ni muda
mrefu wasomi nchini wamekuwa wakipuuza kuisomesha historia ya Zanzibar kwa
kuhofia kutokubalika kwa watu wa aina fulani.
Balozi Seif
amesema hayo katika kongamano la umoja wa wanafunzi wa vyuo vikuu na taasisi ya
elimu ya juu wa CCM wa Wilaya ya Dimani
na kuwataka wasomi wa chama hicho kupiga vita
kasumba hizo kwani bila ya kuielewa historia hawatoweza kuwa wazalendo wa kweli.
Balozi Seif amefahamisha
kuwa iwapo vijana watakubali kujifunza taarifa halisi zilizopita kuhusu Zanzibar
za kabla
na baada ya Mapinduzi ya mwaka 1964 wanaweza
kuwa wanasiasa wazuri wenye kuchanganua mambo kuhusu matukio tofauti.
Amewakumbusha
vijana hao kuelewa matukio ya udhalilishaji yaliyoukumba uchaguzi uliopita
kwa baadhi ya akina mama walilazimika kupewa talaka kwa sababu za itikadi za
kisiasa.
Akizungumzia
kuhusu uchaguzi wa marudio unaotarajiwa kufanyika jumapili ijayo amewatoa hofu
wananchi wa Zanzibar kuwa unatarajiwa kuwa salama na kuwataka mwananchi kuitumia
haki yao ya kupiga kura
Mapema mwenyekiti wa umoja
wa wanafunzi wa vyuo vikuu wilaya ya Dimani Abdulaziz Saleh Khamis ameiomba Serikali
za Tanzania kuhakikisha amani inakuwepo ili
wananchi kuendelea na harakati zake za
kimaisha za kila siku.
Mwenyekiti wa Umoja wa
Wanafunzi wa Vyuo Vikuu na
Elimu ya juu wa Wilaya
ya Dimani Abdulazizi Saleh Khamis
akitoa taarifa ya Umoja
huo
|
0 comments:
Post a Comment