Idara ya Mipango miji na Vijiji Zanzibar kwa
kushirikiana na taasisi mbalimbali za Zanzibar wanatarajia kuanzisha Kituo cha
Mtandao wa Taarifa za Maeneo na mazingira ya Zanzibar ambapo Wananchi
watalazimika kupata taarifa kupitia kituo hicho.
Taarifa hizo zitawekwa katika mfumo wa
kidigitali na kuwekwa katika Mtandao huo ili kuepusha upotoshaji wa taarifa na
pia zipatikane kwa wakati bila ya usumbufu.
Mkurugenzi wa Mipango miji na Vijiji Zanzibar
Dkt. Mohammed Juma ameyasema hayo wakati wa warsha ya kuandaa utaratibu wa
kuanzisha kituo hicho cha Mtandao Shangani mjini Zanzibar.
Amefahamisha kuwa kutokana na kuwepo kwa Vyanzo vingi vya Taarifa zinazohusu Maeneo ya Zanzibar kunapelekea baadhi ya Taarifa hizo kutokuwa sahihi na kupelekea mkanyiko katika jamii.
Amefahamisha kuwa kutokana na kuwepo kwa Vyanzo vingi vya Taarifa zinazohusu Maeneo ya Zanzibar kunapelekea baadhi ya Taarifa hizo kutokuwa sahihi na kupelekea mkanyiko katika jamii.
“Kwa sasa kuna Vyanzo vingi vya kujua maeneo
na mazingira ya Zanzibar..kwa mfano ukienda kutaka taarifa juu ya eneo fulani
inawezekana taarifa hiyo ikatofautiana na Vyanzo vingine lakini tutakapokuwa na
Chanzo kimoja taarifa zitakuwa moja na sahihi”Alisema Dkt Mohamed.
Ametaja faida zitakazopatikana kupitia Mtandao
huo kuwa nipamoja na kuwarahisishia Wananchi kupata taarifa popote walipo na
kwa wakati kinyume na ilivyo sasa ambapo hulazimka kwenda katika Taaisi husika
jambo ambalo huwaletea usumbufu.
Aidha amesema pia itakuwa ni sehemu ya uwazi
kwa Serikali kupitia Taasisi zake ambapo kila kitu kitawekwa wazi na kupatikana
kirahisi kupitia Mtandao huo.
“Mtandao huo utaweka wazi maeneo yote
yakiwemo,Makaazi,maeneo ya uwekezaji..isipokuwa yale yakiusalama ili
kumrahisishia mwananchi kuweza kupata Taarifa bila kuhangaishwa huku na kule”
alibainisha Dkt Mohammed.
Aidha amebainisha kuwa katika Warsha ya kuandaa Mtandao huo Taasisi nane zimeshiriki ili kuwa na sauti moja juu ya maeneo na mazingira ya Zanzibar.
Aidha amebainisha kuwa katika Warsha ya kuandaa Mtandao huo Taasisi nane zimeshiriki ili kuwa na sauti moja juu ya maeneo na mazingira ya Zanzibar.
Amezitaja taasisi hizo kuwa ni pamoja na
Mamlaka ya usimamizi wa ardhi, Idara ya Mazingira, Idara ya Misitu na maliasili
zisizorejesheka na idara ya maendeleo ya uvuvi.
Taasisi zingine ni pamoja na Idara ya
Rasilimali za baharini, Chuo kikuu cha taifa SUZA na Mamlaka ya Mazingira
Zanzibar (ZEMA) ambazo zote zimeshiriki katika Mpango huo wa kuandaa Taarifa za
pamoja.
Jumla ya shilingi Milion 140 zitatumika
kuanzisha Kituo hicho cha Mtandao ambazo ni msaada kutoka Serikali ya Finland.
Kwa upande wake Mwezeshaji wa mafunzo kutoka
Taasisi ya Mazingira ya Finland Bi Riihz Teinirants amesema Taasisi watendaji
wa Taasisi hizo walioshiriki mafunzo wanajukumu la kuwafahamisha wenzao ili
kutimiza lengo lililokusudiwa.
Aidha bi Riihz amesema mbali na kutoa mafunzo
ya kuanzisha Kituo hicho cha Mtandao wataisaidia Zanzibar kutafuta taarifa za
maeneo yake na kuziweka katika Kituo hicho hasa zile za mwambao wa bahari ili
kuleta ufanisi unaohitajika.
Kunzishwa kwa kituo hicho cha Mtandao wa
Taarifa za maeneo ya Zanzibar ni matokeo ya kukamilika kwa Mradi wa kutunza
mazingira Zanzibar (SMOLE) uliofadhiliwa na Serikali ya Finland katika
kuisaidia Zanzibar ambapo Mradi huo ulipata mafanikio makubwa.
Maelezo Zanzibar.
0 comments:
Post a Comment