Wizara
ya Afya Zanzibar kupitia kitengo cha malaria inakusudia kugawa vyandarua
vilivyotiwa dawa 500,000 kwa wananchi mbalimbali ili kujikinga na mbu
wanaoambukiza malaria.
Afisa uhamasishaji
kitengo cha malaria Jokha Salum Hemed amesema vyandarua hivyo vinatarajiwa
kugaiwa kunzia Machi 1 mwaka huu mpango utakaohusisha shehia 82 za Unguja na pemba.
Amesema lengo la utoaji wa vyandarua
hivyo ni kujilinda na maradhi ya malaria nchini.
Amesema serikali
imejidhatiti kuhakikisha inamaliza maradhi ya malaria ambayo yanawaathiri zaidi
wajawaziti na watoto.
Amewataka masheha
kuhakiksha wanorodhesha kaya zote ili kuhakikisha wanapatiwa vyandarua hivyo.
Amewasisitiza wananchi kuendelea kuchukuwa
hatua dhidi ya malaria ikiwemo kuweka safi mazingira yao pamoja na kufukia
vidimbwi vya maji ili kuondoa uwezekano wa mazalia ya mbu.
:zanzibar leo
0 comments:
Post a Comment