Naibu Waziri wa mambo ya ndani wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Hamad Yussuf Masauni amelitaka jeshi la polisi Zanzibar kujipanga vyema juu ya matukio ya uhalifu
yanayojitokeza hasa katika kipindi hichi cha kuelekea uchaguzi wa marudio.
Amesema kumejitokeza matukio ya uhalifu ya
uchomaji wa moto yanayohusishwa na itikadi za kisiasa katika sehemu mbalimbali
hali inayosababisha hofu kwa jamii na mali zao.
Akizungumza na maafisa wa jeshi la polisi katika
ofisi ya makao makuu ya jeshi hilo Kilimani mjini Unguja Masauni amesema ni
vyema jeshi la polisi likajipanga kukabiliana na matukio hayo ili kuhakikisha
nchi inabaki kuwa na amani wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi.
Hata hivyo amelitaka jeshi la polisi
kukamilisha ripoti juu ya mapungufu yaliyotokea wakati wa uchaguzi mkuu
uliopita ili kurekebishwa katika uchaguzi wa marudio.
Nae Kamishna
wa jeshi la polisi Zanzibar Hamdani Omar Makame amesema jeshi hilo limejipanga
vizuri katika kukabiliana na matukio yote ya uhalifu hasa katika kipindi cha
uchaguzi wa marudio wa March 20-2016 na kuhakikisha amani inatawala wakati wote
wa uchaguzi na baada ya uchaguzi huo.
0 comments:
Post a Comment