Afisi
ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Zanzibar inakusudia kufanya utafiti wa mwaka wa
kilimo na mifugo kuangalia kiwango cha
uzalishaji na mapato yatokanayo na sekta hizo Zanzibar.
Mtakwimu
mkuu wa serikali Mayasa Mahfoudh amesema utafiti huo ni miongoni mwa mkakati wa
kimataifa katika kuimarisha takwimu za
kilimo na taarifa zitakazopatikana pia zitaisaidia serikali kupata takwimu
zitakazotumika kuandaa sera na mipango mbali mbali ya maendeleo ya nchi.
Akizungumza
katika mafunzo ya wadadisi watakaofanya utafiti huo amesema uekelezaji wa kazi
watashirikiana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Wizara ya kilimo na Mali asili Zanzibar
Akifungua
mafunzo hayo ya siku tano Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo na Mali asili Affan Othman Maalim amewataka wadadisi hao kuhakikisha wanapata takwimu sahihi
na zinazoaminika zitakazosaidia kufahamu ongezeko la kiwango cha mchango wa
pato la taifa kwa sekta hizo.
Utafiti
huo unategemewa kuanza Febuari 22 mwaka huu na kuchukua siku ishirini ambapo kwa
mujibu wa sensa ya mwaka 2014 sekta ya kilimo inachangia asilimia 27 ya pato la
nchi.
0 comments:
Post a Comment