Wizara
ya Afya Zanzibar imesema vifo vya mama
wajawazito vimepunguwa kutoka 337 hadi 286 kwa kinamama laki moja na watoto wanaokufa
imefikia 29 kati ya elfu kumi wanaozaliwa hadi disemba mwaka 2014.
Mkurugenzi
na Elimu ya Afya Zanzibar Dkt Mohamed Dahoma amesema bado juhudi zaidi zinahitajika
kuweza kufikia lengo la kupunguaza vifo
hivyo kwani vile bado kuna changamoto ya katika jamii na utoaji wa huduma za
afya ya uzazi Zanzibar.
Amezitaja
changamoto hizo ningi zinatokana na maamuzi ya familia na wazee kwa ujumla ikiwemo
kutofatilia taratibu za uzazi salama, kutopanga muda wa matayarisho ya kujifunga na tatizo la usafiri ukifika muda wa
mjamzito kujifungua.
Akizungumza
katika uzinduzi wa mradi wa kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto Dkt
Dahoma amefahamisha kuwa mradi huo wanalenga unalenga kukabiliana na changamoto
hizo kwa kuimarisha utoaji wa huduma stahiki za afya kwa karibu zaidi.
Amesema
mradi huo wa miaka miwili unaojulikana Afya bora ya Mama na Mtoto kwa maendeleo endelevu utawafikia wajawazito
elfu 45 na watoto elfu 75 katika shehia 286 za Zanzibar unagharimu zaidi ya
shilingi bilioni 23 ikiwa ni ufadhili wa
Serikali ya Canada na unaratibiwa na shirika la kimataifa la Save the children.
Kazi
kuu za mradi huu ni kusimamia mama wajawazito kufuatilia huduma za afya,
kujitayarisha katika kipindi cha kujifungua na ufuatiliaji watoto hadi katika
wiki ishirini na tatu za kuzaliwa kwa vile utaishirikisha jamii katika
kusimamia huduma hizo za wazazi.
Akizindua
mpango huo ulioenda sambamba na mafunzo kwa watendaji wa afya ya uzazi Naibu Katibu
Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Halim Ali Maulid amewataka watendaji wa sekta hiyo
kuacha kufanya kazi kisiasa kwani kunachangia kukwamisha kufika malengo ya utoaji
wa huduma kwa jamii na utekelezaji wa malengo ya miradi kadhaa inayoanzishwa
katika sekta hiyo.
Amesema
ni vyema kubadilika kwa vile sekta ya afya sasa inalaumiwa kwa kuwa na utendaji
mbaya wa kazi usiofuata maadili hivyo ni vyema kubadilika kwani wao hawako
katika kuchezea maisha ya watu.
“Acheni
kucheza na maisha ya watu kama huwezi kufanya kazi acha na kama siasa basi
nenda huko si kuingiza masuala hayo katika kazi haipendezi”. amesema Naibu
Halima.
Amesema
kuanzishwa kwa mradi huo ni hatua muhimu ya kuweza kufikia malengo ya serikali
ya kupunguza vifo hivyo vya mama wajawazito na watoto ambavyo vingi vyanzo
vyake vinavyotokana na uzembe vinaweza kuzuilika iwapo kutatolewa huduma bora
na elimu kwa jamii, familia, wazee na wanandoa wenyewe.
Halima
amefahamisha kuwa kufanikiwa hilo mradi huo utafikia lengo na kuwa mfano katika
utekelezaji wake hali inayoweza kuongeza ushawishi kwa wafadhili kuendelea
kusaidia masuala ya uzazi n malezi salama ya mototo Zanzibar.
Meneja mradi wa Afya bora ya Mama na Mtoto kwa maendeleo
endelevu Zanzibar kutoka Save the childrens Dkt Bernard mbwele
akitoa mada juu ya mradi huo
0 comments:
Post a Comment