TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa mabalozi
watatu katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda
na Kimataifa.
Rais Magufuli pia
amefanya uteuzi wa makamishna wanne wa Jeshi la Polisi na Kaimu Mkurugenzi Mkuu
wa Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Taarifa ya Katibu Mkuu
Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, imewataja mabalozi walioteuliwa kuwa ni Dkt.
Asha-Rose Mtengeti Migiro, Mheshimiwa Mathias Meinrad Chikawe na Dkt.
Ramadhan Dau.
Vituo vya uwakilishi
kwa mabalozi hawa vitajulikana baada ya taratibu husika za kidiplomasia
kukamilika.
Kwa upande wa
Makamishna wa Polisi, Balozi Sefue amewataja walioteuliwa kuwa ni:
1.
Naibu Kamishna wa Polisi Simon Nyakoro Sirro ambaye
amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi, na ameteuliwa kuwa Kamanda wa Polisi
Kanda Maalum ya Dar es salaam. Kamishna Sirro anajaza nafasi
iliyoachwa wazi na Kamishna Mstaafu Suleiman Kova.
2.
Naibu Kamishna wa Polisi Albert Nyamuhanga ambaye
amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi na ameteuliwa kuongoza Idara ya
Fedha, Utawala na Lojistiki.Kamishna Nyamuhanga anajaza nafasi
iliyoachwa wazi na Kamishna wa Polisi Clodwing Mathew Mtweve aliyeteuliwa kuwa
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza.
3.
Naibu Kamishna wa Polisi Robert Boaz Mikomangwa ambaye
amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi na ameteuliwa kuongoza Idara ya
Intelijensia. Kamishna Mikomangwaanajaza nafasi iliyoachwa wazi na
Kamishna Valentino Mlowola aliyeteuliwa kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).
4.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Nsato Marijani
Mssanzya ambaye amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi na
ameteuliwa kuongoza Idara ya Mafunzo na Operesheni. Kamishna Mssanzya anajaza
nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna wa Polisi Paul Moses Chagonja aliyeteuliwa
kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi.
Aidha, Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Modestus
Francis Kipilimba kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Vitambulisho vya Taifa (NIDA). Kabla ya Uteuzi huu Dkt. Kipilimba alikuwa
Mkurugenzi wa Menejimenti ya Udhibiti (Director of Risk Management)
katika Benki Kuu ya Tanzania. Dkt. Kipilimba anajaza nafasi
iliyoachwa wazi na Bw. Dikson Maimu ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
Teuzi zote zinaanzia
leo tarehe 15 Februari, 2016.
hii hapa taarifa kamili sikiliza
hii hapa taarifa kamili sikiliza
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
15 Februari, 2016
0 comments:
Post a Comment