April 26, 2014


Watanzania wamesherehekea miaka 50 yaMmuungano wa Ttanganyika na Zanzibar kwa amani huku Rais Jakaya Kiwete akiwaongoza wananchi katika kilele cha maadhimisho hayo katika uwanja wa uhuru jijini daresalaam.

Sherehe hizo ziliambatana na maonyesho mbalimbali yakiwemo ya kijeshi na halaiki zilihudhuriwa na viongozi wa nchi 35 wakiwemo marais wa nchi 11 na mashirika ya kimataifa.

Akiwatambulisha viongozi waliohudhuria sherehe hizo Rais wa Kikwete amewasisitiza watanzania kuthamini maendeleo ya muungano kutokana na mafaniko yaliyopatikana.

Amefahamisha kuwa sherehekea hizo ni kuwakumbuka waasisi wa Tanganyika  na Zanzibar m mwalimu nyerere na sheikh abeid amani karume huku pia inatathmini maendeleo yaliyofikiwa katika kipindi hicho.

Amesema muungano huo wa April 26 1964  kufikia nusu karne ni ishara kubwa ya kuleta mabadiliko katika Tanzania na bara la Afrika kwa pamoja.



 

0 comments:

Post a Comment