Vijana wengi Zanzibar wanashindwa
kutumia fursa za ajira zilizopo kutokana na
ukosefu wa taaluma na uwezo wa kuzifia fursa hizo.
Afisa kutoka Wizara ya ustawi wa
jamii maendeleo ya wanawake na watoto Zanzibar
Zeyana Ahmed Kassim
amesema ajira hizo zinapatikana
katika sekta ya uvuvi, utalii, kilimo, biashara na elimu na bado hawajapewa kipaumbele
na kundi hilo.
Amewataka vijana kufanya utafiti
wa makini juu ya fursa hizo ili kuondokana na utegemezi wa ajira kutoka
serikalini.
Zeyana alikuwa akizungumza katika
jukwaa la majadiliano yaliyolenga kuimarisha mawasiliano baina ya vijana na Serikali
katika kuzifikia ajira Mjini Zanzibar.
Nao vijana hao wameiomba serikali
kubadili mfumo wa kuendelea kuwarudisha wastaafu kazini inawanyima fursa
vijana nafasi hizo.
0 comments:
Post a Comment