February 08, 2016

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimjulia hali Mufti Mkuu wa Tanzania
Sheikh Abubakar Zubeiry aliyelazwa kwa matibabu katika taasisi ya Moyo
ya Jakaya Kikwete katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.Pamoja naye
ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee
Mhe Ummy Mwalimu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali,
Mhe George Masaju pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mkuu
wa Taasisi hiyo Profesa Mohamed Janabi
leo Jumatatu February 8, 2016.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisindikizwa wakati wa kuondoka baada
ya kumjulia hali Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeiry aliyelazwa
kwa matibabu katika taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete katika
hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Pamoja naye ni Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee
Mhe Ummy Mwalimu na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa
Taasisi hiyo Profesa Mohamed Janabi.
(Picha na Ikulu)

0 comments:

Post a Comment