Makamo
wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema uchaguzi wa
marudio upo na bajeti yake imeshatengwa na wanachosubiri ni
mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi Zanzibar atangaze tarehe ya kufanya
uchaguzi huo.
Amesema
bajeti hiyo haitatofautiana na ile iliyotumika katika uchaguzi wa Novemba 2015 iliyofikia
karibu ya shilingi bilioni saba.
Amekanusha
kauli kuwa uchaguzi huo hautafanyika kwa vile matokeo yanayolazimisha
kutangazwa na CUF yameshafutwa kwa mujibu wa sheria kutokana na kasoro kadhaa
zilizojitokeza.
Akizungumza
na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya miaka 52 ya mapinduzi Balozi Seif amesema
mazungumzo yanayoendelea ni ya kuhakiksha amani inaimarika Zanzibar na si suala
la uchaguzi uliofutwa.
Akizungumzia
kuhusu maadhimisho ya miaka 52 sherehe za Mapinduzi Balozi Seif amewabeza
wanaosusuia sherehe hizo kwa madai kuwa Rais Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein
kuwa si halali ni upotoshwaji mkubwa.
Amefahamisha
kuwa rais yupo kihalali na hata mawaziri wake wote na watamaliza ukomo wao hadi
atakapoapishwa rais mwengine kama ilivyoanishwa katika katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 na si kama inavyeleezewa
kuwa ukomo wake umeisha tangu tarehe 2 Novemba.
0 comments:
Post a Comment