Wakazi
watano wa Zanzibar wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka
ya kusafirisha kobe 201 aina ya India wenye thamani ya Sh30 milioni.
Wakili
wa Serikali Ester Martin akishirikiana na Neema Mwanga, aliwataja washtakiwa
hao kuwa ni David Mungi (36), Mustafa Bakar (43), Mohammed Seleman (43), Salum
Wakili (30) ambao ni wafanyabiashara na mvuvi, Shaban Haji (45).
Wakili
Martin alidai kuwa kati ya Novemba 1 na 16 katika maeneo tofauti jijini Dar es
Salaam na Zanzibar, washtakiwa hao kwa pamoja walisafirisha nyara za Serikali
kinyume cha sheria ya wanyama pori.
Ilidaiwa
kuwa Novemba 16 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA),
washtakiwa hao walikamatwa na kobe hao.
Alidai
kuwa washtakiwa Seleman, Wakili na Haji wanadaiwa kuwa katika kipindi hicho
katika maeneo tofauti walipokea na kusafirisha nyara hizo bila ya kibali cha
wanyama pori.
Baada
ya kusomewa mashtaka hayo, upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi bado
haujakamilika na washtakiwa hawakuruhusiwa kuongea chochote kwa kuwa mahakama
hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi hadi watakapofikishwa
Mahakama Kuu baada ya upelelezi kukamilika.
Hakimu
Mkazi, Respicius Mwijage aliahirisha kesi hadi Desemba 14 na kuwashauri
washtakiwa kuwasilisha maombi ya dhamana Mahakama Kuu.
Washtakiwa
hao walirudishwa rumande
0 comments:
Post a Comment