Rais wa Zanzibar na
mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dr Ali Mohmaed Shein Serikali imepania kuhahakisha
sheria zinafuatwa na imekusudia kuchukuwa hatua kali kwa wanaozikiuka.
Amesema katika miaka
mitano iliyopita sheria nyingi na kali zimepitishwa kama vile za uhujumu uchumi
na sheria ya maadili ya viongozi.
Hivyo Dk Shein amewataka
wafanyabishara na viongozi wenye dhamana kuzitekeleza ipasavyo na si suala la
kuelezewa kila mara.
Alikuwa akijibu
namna Serikali inavyo chukuwa hatua katika kuendana na kasi ya kupambana na
maovu katika jamii hasa ufisadi katika ziara fupi ya kutembelea eneo
litakalojengwa bandari mpya ya Mpigaduri.
Rais shein ameeleza kuwa
mradi huo unaotarajiwa kuanza mwanzoni mwa mwaka 2016 pamoja na ule wa upanuzi
wa kiwanja cha ndege cha Abeid Amani Karume ni hatua muhimu ya kuongeza kasi ya
kukua uchumi na kuharakisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii Zanzibar.
Ujenzi wa bandari mpya ya Mpigaduri utakuwa
wa awamu tatu ambapo awamu ya kwanza ya ujenzi huo utagharimu Dola za
kimarekani milioni 231.4 itaanza mwezi Januari, 2016 na itajengwa na Kampuni ya
CHEC kutoka nchini China.
“Huu
ni mradi mkubwa kwa uchumi wetu hivyo wananchi watarajie maendeleo makubwa na
yenye kasi zaidi ya uchumi wetu” Dk. Shein alieleza.
Amewaambia waandishi
wa habari na viongozi waliokuwepo kuwa mradi huo wa ujenzi wa bandari ya
Mpigaduri si mradi mpya ulianza tangu Awamu iliyoongozwa na Dk. Salmin Amour na
awamu hii ndio umefanikiwa kufikia hatua
ya utekelezaji.
“Sisi
awamu hii tumekwenda mbele zaidi,tumetafuta fedha na tumefanikiwa kutokana na
urafiki wetu na serikali ya Jamhuri ya Watu wa China tutapata mkopo wa kujenga
bandari hii” Dk. Shein alidokeza.
0 comments:
Post a Comment