December 03, 2015


Studio ya redio Hits Fm iliyopo Migombani Zanzibar imechomwa moto na kundi la watu walisiojulikana.
Tukio hilo limetokea jana majira ya 7:30 usiku ambapo watu hao zaidi ya 15 walivamia studio hiyo wakiwa na silaha na walikuwa wamejifunika nyuso zao waliwatisha walinzi na baadae kumpiga mwandishi Ali Abdallah aliekuwa zamu studio.
Bado haijulikana chanzo cha studio za Hits fm kuchomwa moto na kusabisha hasara inayokadiriwa kuwa ni zaidi ya shilingi milioni 70 ila Jeshi la Polisi wanaendelea na uchunguzi.

0 comments:

Post a Comment