Ujumbe wa
Waangalizi wa Uchaguzi wa Umoja wa Ulaya
Tanzania
– Uchaguzi Mkuu 2015
Taarifa
kwa Vyombo vya Habari
Tarehe:
08/12/2015
Ya kutolewa mara moja
Dar
es Salaam, 8 December2015
Ujumbe wa Waangalizi wa Uchaguzi wa Umoja wa
Ulaya (EU EOM) kwa Tanzania unatoa tena wito kwa ukamilishwaji haraka wa
mchakato wa uchaguzi Zanzibar kulingana na kanuni za chaguzi shirikishi, za
uwazi, zinazotekelezwa kwa wakati na za kuaminika.
Kufuatia Siku ya Uchaguzi tarehe 25 Oktoba,
Ujumbe wa Waangalizi wa Uchaguzi wa Umoja wa Ulaya umebaki nchini kufuatilia
chaguzi zilizoahirishwa Tanzania Bara na mchakato uliyositishwa Visiwani
Zanzibar, baada ya tamko la Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) la
tarehe 28 Oktoba, lililofuta matokeo ya uchaguzi mkuu Zanzibar.EU EOM ilikutana
na wadau wakuu Visiwani, vikiwemo vyama vya siasa, Mwana Sheria Mkuu wa
Serikali wa zamani na wa sasa, wadau wa sharia na mahakama, asasi za kiraia na
maafisa uchaguzi. Bahati mbaya EU EOM haikuweza kukutana na Mwenyekiti wa ZEC.
EU EOMinafahamu kuhusu mazungumzo yanayoendelea
kati ya CCM na CUF, yanayowashirikisha Marais Wastaafu wa Zanzibar. EU EOM
inarudia tena wito uliyotolewa kwa pamoja na jumbe zingine za uangalizi za
kimataifa tarehe 29 Oktoba, unaoishauri ZEC kuonyesha uwazi kamili kufuatia
uamuzi wake wa kufuta uchaguzi na uongozi wa kisiasa Zanzibar kuweka maslahi ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ya Zanzibar kwanza, kwa lengo la ukamilishwaji haraka wa
mchakato wa uchaguzi, kulingana na kanuni za kidemokrasia za chaguzi pamoja na
sheria zaZanzibar.
“EU EOM imekuwepo
nchini tangu 11 Septemba kufuatilia mchakato wa uchaguzi ndani ya Muungano na Zanzibar.
Idadi kubwa ya waangalizi 141 wa EU nchini walirejea Ulaya katikati ya mwezi
Novemba, lakini timu ndogo ya watathmini wa uchaguzi ilibaki nchini kufuatilia
ngazi zilizobaki za mchakato wa uchaguzi,” alisema Muangalizi Mkuu wa EU EOM,
Judith Sargentini.
“Japokuwa mchakato wa uchaguzi Zanzibar
haujakamilika,EU EOM itarejea Ulaya kwa muda tarehe8 Desemba.Umoja wa Ulaya
unaendelea hata hivyo, kuunga mkono kikamilifu mchakato wa uchaguzi Zanzibar na
kwa mchakato mpana zaidi wa kidemokrasia Tanzania.EU EOM iko tayari kurejea na
kuangalia mchakato wa uchaguzi Zanzibar pindi makubaliano ya kuendelea na
mchakato huo yanayolingana na chaguzi shirikishi, za uwazi, zinazotekelezwa kwa
wakati na za kuaminika yatakapofikiwa,”aliongeza Muangalizi Mkuu.
EU EOM ilitumwa kufuatia mialiko toka Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Tume ya Uchaguzi
Zanzibar.EU EOM inapenda kutoa shukrani zake kwa NEC kwa kuiongezea muda wake
kupita muda uliyopangwa awali, jambo linaloashiria upana wawigo na mamlaka ya
EU EOM, ambayo yanahusisha zaidi ya uangalizi wa muda mfupi.Ujumbe ulitoa tamko lake la awalila mchakato wa uchaguzi tarehe 27 Oktoba. Tarehe29 Oktoba,EU
EOM, pamoja na jumba zingine za waangalizi za kimataifa za Umoja wa Afrika,
SADC na Jumuiya ya Madola, ilitoa tamko la pamojakuhus Zanzibar.EU EOM itawasilisha ripoti
kamili ya kina, ikiwemo mapendekezo kwa chaguzi zijazo,ndani ya miezi mitatu ya
kukamilika kwa mchakato wa uchaguzi.
0 comments:
Post a Comment