December 29, 2015

Serikali imepoteza jumla ya Shilingi  bilioni 48.47 baada ya makontena 11,884 na magari 2,019 kupitishwa badarini Dar es Salaam bila kulipiwa kodi.  
Kufuatia kashfa hiyo watu 7 wanashikiliwa na wengine 8 wanatafutwa na Jeshi la Polisi kwa kuhusishwa na ukwepaji kodi huo uliolikosesha taifa mapato.
Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema ufisadi huo umebainika baada ya serikali kuzifanyia ukaguzi bandari zote za nchi kavu (ICDs) jijini Dar es Salaam.
Akifafanua  Waziri Mbarawa amesema makontena hayo 11,884 yalikuwa na thamani ya Sh 47.4 bilioni wakati magari gari 2019 zenye thamani ya sh 1.07bilioni yalitolewa bandarini pasipo kulipiwa.

0 comments:

Post a Comment