December 21, 2015

Shirika la biashara la taifa la Zanzibar ZSTC limefanikiwa kununua tani  1730 za karafuu  zenye thamani ya  shilingi bilioni 24.2.
Karafuu hizo zimenunuliwa  kuanzia  Julai 9 hadi Disemba 18 mwaka huu kwa wakulima mblimabli wanaozlisha zao hilo.
Mkurugenzi wa ZSTC mwanahija almasi ali  amekanusha madai kuwa shirika hilo  halina  fedha za kununulia karafuu na badala yake linatoa risiti za malipo kwa wakulima  si ya kweli.
Amefahamisha kuwa ZSTC ina fedha za kutosha za kununulia  karafuu katika kipindi chote cha manunuzi na hakuna mu atakae kopwa fedha zake.

Kuhusu kuweka alama zao hilo (BRANDING) amesema  taratibu za mpango huo zimeshakamilika na wakati wowote inaweza kutumika.

0 comments:

Post a Comment