December 28, 2015

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt. John Pombe Magufuli amewaapisha Mawaziri aliowateuwa hivi karibuni kukamilisha baraza lake la mawaziri.
Katika hafla hiyo iliyofanyika Ikulu jijini Dar-es-salaam waliapishwa ni Prof Jumanne Abdalah Magembe Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt Joyce Ndalichako Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, na Waziri wa Fedha Mipango Dkt Philip Isdori Mpango.
Wengineo ni   waziri wa maji na umwagiliaji Mhandisi Gerson lwenge,  Prof Makame Mnyaa Mbarawa Waziri wa ujenzi uchukuzi na Mawasiliano na Hamad Masauni Yusuph Naibu Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi.
Mawaziri hao baada ya kuapishwa wameeleza kuwa watafanya kazi sambamba na kasi na kauli mbiu ya hapa kazi tu kwa kuzingatia wizara watakazoziongoza kuwa ni nyeti na za msingi kwa uchumu na maendeleo ya Tanzania.

Baadhi ya mawaziri hao waliwasili wizarani mwao muda mfupi baada ya kuapishwa na kufanya vikao na viongozi na watendaji ili kujitambulisha.





0 comments:

Post a Comment