Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli amemalizia kujaza nafasi za uteuzi wa Mawaziri na Naibu
Waziri alizobakiza wakati akitangaza baraza la Mawaziri la kwanza katika awamu
ya tano yautawala wake
Uteuzi huo ni kama ifuatavyo;
1. Profesa Jumanne Maghembe -Ameteuliwa kuwa
Waziri wa Maliasili na Utalii.
2. Dkt. Philip Mpango – Ameteuliwa kuwa Waziri
wa Fedha na Mipango (Ni baada ya kumteua kuwa Mbunge).
3. Mhandisi Gerson Lwenge – Ameteuliwa kuwa
Waziri wa Maji na Umwagiliaji.
4. Dkt. Joyce Ndalichako – Ameteuliwa kuwa
Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi.(Ni baada ya kumteua kuwa Mbunge)
5. Mheshimiwa Hamad Masauni – Ameteuliwa kuwa
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
6. Prof. Makame Mbarawa –Amehamishwa kutoka
Wizara ya Maji na Umwagiliaji na kwenda Wizara ya Ujenzi, uchukuzi na
Mawasiliano
Katika hatua nyingine Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewatakia heri watanzania wote
katika Sikukuu za Maulid, Christmas na Mwaka Mpya na kuwataka washerehekee kwa
amani na utulivu.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa
Mawasiliano, IKULU
23 Desemba, 2015
0 comments:
Post a Comment