Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kutunza na
kulinda Utamaduni wa Zanzibar na kuyafanyia matengenezo majengo ya
Mji Mkongwe yaliyochoka kwa ushirikiano wa Mfuko wa Kimataifa wa
kuyaendeleza majengo ya Miji Mikongwe Duniani na kuyatunza {World
Monument Fund}.
Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Habari, Utamaduni,Utali na Michezo Issa Mlingoti wakati akifungua mkutano kwa
niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo wa kutembelea na kuzungumzia namna ya
kuyafanyia matengenezo majumba mabovu ili yasitoweke katika Mji huo.
Amese matengenezo hayo hufanywa kwa mashirikiano ya
pamoja kati ya Serikali, wahisani na Mashirika mbalimbali ya Kimataifa.
Nae Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mji Mkongwe
Zanzibar Issa Makarani amesema hivi sasa kuna majengo yapo hatarini
kupotea katika urithi wa Kimataifa kutokana na kuchakaa na kufikia
hatua ya kuanguka hivyo kutokea mfuko huo kusaidia ni jambo la faraja.
Aidha alisema wananchi kwa upande wao
wanalazimika kufuata kanuni na taratibu za kuuhifadhi na kuulinda Mji
Mkongwe wa Zanzibar ikiwamo kuacha kupitisha magari makubwa ambayo hupelekea
kupasuka kwa majengo.
“Kuazia mwakani kutakua na sheria maalumu ya kupitisha vyombo
vya moto katika maeneo ya Mji Mkongwe wa Zanzibar ambayo madereva watalazimika
kuifuata,” alisema Makarani.
0 comments:
Post a Comment