December 10, 2015


Jeshi la polisi Mkoa wa kusini Pemba limetakiwa kuzisimamia kikamilifu kesi 27 zilizobakia za makosa ya udhalilishaji zilizopo mahakamani ili kupatia hukumu kwa  mujibu wa sheria.
Amesema ni jambo la kusikitisha kwa kesi 64 za udhalilishaji zilizoripotiwa katika kituo cha mkono kwa mkono Disemba 2014 hadi mwezi huu wa Disemba  2015 kesi 13 tu zimehukumiwa na kesi 27 zikiendelea mahakamani huku kesi 24 zimeshafutwa mahakamani.
kauli hiyo ameitolewa na Mkuu wa wilaya ya Chake Chake Hanuna Ibrahim Masoud amelitaka katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto.
Kamanda wa polisi Mkoa wa kusini Pemba Mohamed Sheikhan Mohamed ameahidi kuzisimamia kesi hizo kupatiwa hukumu sambamba na kuvikomesha vitendo hivyo.
Hata hivyo amesema ili lengo la kudhibiti vitendo vya udhalilishaji wa wanawake na watoto liweze kufanikiwa lazima kuwe na nguvu ya pamoja kati ya jeshi hilo, afisi ya Mkugenzi wa mashtaka, Mahakama na wananchi.
mapema mwenyekiti wa mtandao wa polisi wanawake walioandaa maadhimisho hayo Asha Tahir Silima amesema mtandao huo unaendelea kutoa elimu katika ngazi mbali mbali kuhusu makosa ya udhalilishaji pamoja na kuimarisha huduma za dawati.

0 comments:

Post a Comment