Katibu Mkuu wa zamani wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa amesifia
kasi ya rais John Magufuli hasa katika kupambana na ufisadi nchini.
Dk. Slaa amesema kuwa alichowahi kukizungumzia awali
kimetimia kwa kuwa nchi hii ilihitaji mtu kama Magufuli.
“Nadhani sasa unaelewa niliposhikilia msimamo wangu. Katika
mazingira ya sasa Magufuli ni bora zaidi. Niliwahi kusema kuwa hii nchi kwa
siku za mwanzo inahitaji udikteta kuirudisha kwenye mstari ulioonyooka,
nimefurahi sana,” Dk.
Slaa ameliabia gazeti la Raia Mwema.
Amesema kuwa Bunge linatakiwa kufanya kazi ya kuudhibiti
udikteta huo ili usivuke mipaka lakini limuunge mkono kwa hatua anazochukua.
Katika hatua nyingine, Dk. Slaa amemshauri Rais Magufuli kuiangalia
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na kuifumua.
“Pasipo kuchukua hatua ya kuifumua Takukuru, sina hakika
kama matarajio yatafikiwa,” alisema
Dk Slaa na kuongeza kuwa hatua hizo zinapaswa kuchukuliwa haraka.
0 comments:
Post a Comment