Bodi ya mapato Zanzibar ZRB imeifunga ofisi ya kampuni ya simu ya VODACOM
kwa kushindwa kulipa kodi kuanzia Disemba 2014 hadi Juni 2015.
Afisa uhusiano wa bodi hiyo Makame
Khamis Mohamed amesema kamupini hiyo ilipaswa kuwasilisha marejesho yao na
malipo chini ya 30 Novemba lakini hawakufanya hivyo wakati taarifa
wamepelekea hadi kwa maandishi.
Amesema Vodacom kama kampuni
nyengine zilizopo Zanzibar wanawajibika kulipa kodi kwa mujibu wa sheria ya
kodi namba 7 ya 2009 na sheria 4 ya kodi ya ongezeko la thamani ya 1998.
Makame amefahamisha kuwa kutokana na hali
hiyo ZRB imelazimika kuchukua uamuzi huo kutokana na vodacom kushindwa kuwasilisha
marejesho yao bila ya taarifa yeyote
Nae mwakilishi wa Vodacom upande wa Zanzibar
Mohamed Mansour amesema suala hilo liko nje ya uwezo wao kwa kuwa kuna
miingiliano ya usimamizi wa kodi kati ya serikali ya Tanzania na ya Zanzibar.
Amefahamisha kuwa kutokana na hali
hiyo kampuni hiyo imekuwa ikilipa moja kwa moja mamlaka ya mapato Tanzania TRA hivyo ni vizuri ZRB kudai huko.
Hata hivyo Mansour amesema kwa sasa
wanafanya juhudi za kufanya mazungumzo na tra kutatua tatizo hilo linalo
wakwamisha kuanya kazi kwa ufanisi.
0 comments:
Post a Comment