Wabunge
wa vyama vya upinzani vinavyounda Ukawa wameonywa kutofanya jambo lolote
litakaloashiria kuvuruga Bunge wakati Rais John Magufuli atakapolihutubia leo
jioni.
Akiongea
mjini Dodoma, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM ambaye pia ni Mbunge wa jimbo
la Mtama, Nape Nnauye amesema Wabunge hao wa Ukawa wanapaswa kufahamu kuwa
kitendo chochote watakachofanya kwa lengo la kuvuruga hotuba hiyo ni kinyume
cha sheria na taratibu za Bunge na hawatavumiliwa.
Nape
alionesha kuwashangaa wabunge hao kudai kuwa hawamtambui Rais Magufuli ili hali
wanashiriki katika shughuli zote za Bunge ikiwa ni pamoja na kumpigia kura
Waziri Mkuu ambaye ameteuliwa na Rais huyohuyo wanaedai hawamtambui.
Wabunge
wa Ukawa juzi walieleza kuwa
hawatakubali kumuona Rais wa Zanzibar, Dkt Ali Mohamed Shein akiingia katika
Bunge hilo leo kwa kuwa kipindi chake cha urais Zanzibar kimekwisha.
Wabunge
hao pia walisema pia wamemuandikia barua Spika wa Bunge kuhoji uhalali wa
hotuba ya Rais wakati Zanzibar bado haijampata Rais mpya.
0 comments:
Post a Comment