November 20, 2015

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli, amemuapisha Majaliwa Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania.
Majaliwa anakuwa waziri mkuu wa kumi na moja wa Tanzani ameapishwa baada ya Bunge kuthibitisha uteuzi wake hapo jana.
Hafla ya Kuapisha  Majaliwa imefanyika kwenye Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wa serikali wakiwemo, Makamu wa Rais wa Tanzania, Samia Hassan Suluhu, Rais wa Zanziba, Dk. Ali Mohammed Shein, Makamu wa Rais Mstaafu, Dk. Gharib Bilal, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai na Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson, Wabunge, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Davis Mwamunyange na Wabunge.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa Kassim baada ya kuapishwa  rasmi kushika wadhifa wake huo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma leo.
Makamo wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa Kassim baada ya kuapishwa katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma leo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Makamo wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan (kushoto) na Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa Kassim (kulia) baada ya kuapishwa rasmi kushika wadhifa huo katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma leo,]Picha na Ikulu.]

0 comments:

Post a Comment