Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, Vijana, Wanawake na
Watoto Msham Abdalla Khamis amewashauri watendaji wa vyombo vya sheria kutatua changamoto zinazokwamisha kesi za
ukatili na udhalilishaji wa kijinsia ili kuwatia hatiani watuhumiwa wa vtendo
hivyo kwa mujibu wa sheria.
Amesema bado tatizo hilo ni kubwa na taifa
linapata hasara kubwa ya kuharibiwa watoto ambao ni rasilimali ya taifa na wengi
wao huathirika kisaikolojia na kupata matatizo makubwa ya kiakili.
Akifungua
warsha ya kuwajengea uwezo wadau hao wa kushughulikia kesi za ukatili na
udhalilishaji wa kijinsia Zanzibar amesema kutochukuliwa hatua za kisheria kwa
wakati muafaka kunawafanya watuhumiwa wa
makosa hayo kujenga kiburi na kusabisha kuongezeka kwa makosa hayo.
Nao
watendaji hao wa vyombo vya sheria Zanzibar wamesema yapo matatizo mengi
yanayosababisha kesi nyingi za aina hiyo kukwama kusikilizwa ama kumalizwa
kinyeji , ikiwemo kutokufika mashahidi muhimu Mahakamani au watu kusameheyana.
Wamesema
kazi inayotakiwa kutiliwa mkazo ni kutoa elimu kwa jamii na ili wawe tayari kutoa
ushahidi mahakamani utakao mtia hatiani mtuhumiwa na kupewa adhabu kubwa inayomstahikia.
Mafunzo
hayo yametayarishwa na Wizara ya Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, Vijana, Wanawake
na Watoto na kuwashirikisha watendaji mbali mbali wa vyombo vya sheria ikiwemo
Polisi katika madawati ya kijinsia, Mahakimu, Afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka
na watendaji wengine wa Wilaya na Mkioa wa Wizara hiyo.
0 comments:
Post a Comment