November 21, 2015

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akipata maelezo kutoka kwa  Kaimu Mkurugenzi wa mamlaka ya Mji Mkongwe wa Zanzibar Mussa Awesu Bakari wakati akiangalia ramani ya Mradi wa ujenzi wa Ukuta wa Forodhani Mjini Unguja akiwa katika ziara maalum ya kutembelea maendeleo ya Miradi mbali mbali Mjini  Unguja.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akipata maelezo ya ramani ya ujenzi wa Mtaro wa maji ya Mvua katika viwanja wa mnazi mmoja kutoka kwa Mhandisi wa Manispaa ya Zanzibar Mzee Khamis Juma wakati alipotembelea mradi huo wa ujenzi unaojengwa na kampuni ya CRJ kutokaChina.


picha: ikulu

0 comments:

Post a Comment